Wapigajai jihadi 44 wapatikana wamekufa katika jela Chad
19 Aprili 2020Akizungumza katika televisheni ya taifa, Youssouf Tom amesema wafungwa 44 walikutwa wamekufa katika chuma walimofungiwa siku ya Alhamis.
Uchunguzi uliofanywa kwa watu wanne miongoni mwa waliofariki umeonesha aina ya kitu hatari ambacho kimesababisha matatizo ya moyo katika baadhi ya waliofariki pamoja na matatizo makubwa ya kupumua kwa wengine, amesema.
Waliofariki walikuwa miongoni mwa kundi la washukiwa 55 waliokamatwa katika wakati wa operesheni kubwa ya jeshi katika eneo la ziwa Chad iliyoanzishwa na rais Idriss Deby Itno mwishoni mwa mwezi Machi.
"Kufuatia mapigano katika eneo la ziwa Chad, wanachama 58 wa kundi la Boko Haram walikamatwa na kupelekwa N'Djamena kwa ajili ya uchunguzi zaidi," amesema Tom.
"Siku ya Alhamis asubuhi, waliowafunga walituambia kuwa wafungwa 44 wamekutwa wamefariki katika chumba walimokuwa," Tom alisema, na kuongeza kuwa alifika katika eneo hilo.
Chanzo cha vifo hakijajulikana
"Tumezika miili 40 na kupeleka miili minne katika uchunguzi wa kitabibu kwa ajili ya kujua chanzo cha vifo hivyo." Uchunguzi unaendelea kubaini kile kilichotokea kwa wafungwa hao hadi wakafariki, alisema.
Duru za usalama, zikizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina kililiambia shirika la habari la AFP kuwa "wafungwa hao 58 waliwekwa katika chumba kimoja na hawakupewa kitu cha kula ama kunywa kwa siku mbili".
Mahamat Nour Ahmed Ebedou, katibu mkuu wa chama cha ulinzi wa haki za binadamu nchini Chad, (CTDDH), ametoa shutuma kama hizo.
Maafisa wa jela waliwafunga wafungwa hao katika chumba kidogo na hawakuwapa chakula ama maji kwa siku tatu kwasababu walikuwa wanashutumiwa kuwa katika kundi la Boko Haram", Ebedou aliliambia shirika la habari la AFP. "Ni unyama kile kilichotokea."
Serikali imekana madai hayo.
"Hakukuwa na kuwatendea vibaya," Waziri wa sheria wa Chad , Djimet Arabi, ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu.