Watu 32 wauwawa katika mapigano ya kikabila Sudan
20 Novemba 2023Matangazo
Bulis Koch, Waziri wa habari wa eneo la Abyei amesema siku ya Jumapili asubuhi kundi la vijana la Twic Dinka linaloungwa mkono na wanamgambo wa ndani lilivishambulia vijiji vya watu wa kabila la Ngok Dinka Kaskazini Mashariki mwa mji wa Agok.
Soma pia:Ujumbe wa UN watakiwa kumaliza shughuli zake Sudan
Msemaji wa jeshi la Sudan hakujibu ombi la Reuters kutaka maoni juu ya taarifa hii. Sudan Kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe muda mfupi baada ya Sudan kujipatia Uhuru wake mwaka 2011.
Makubaliano ya amani yaliyosainiwa miaka mitatu iliyopita inaendelea kuwepo lakini serikali ya mpiti imekuwa ikichukua hatua ndogo ya kuunganisha makundi kadhaa ya jeshi.