Wawaniaji watatu wa Ballon d'Or watangazwa
2 Desemba 2015Watakaowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Lionel Messi wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona na Mbrazil Neymar da Silva Santos Júnior wa pia wa Barcelona, anayeingia katika kinyang'anyiro hicho kwa mara ya kwanza.
Wanaochuana kuwania tuzo ya Mchezaji bora mwanamke ni kiungo wa timu ya taifa ya Marekani Carli Lloyd, Aya Miyama wa Japan na Celia Sasic wa Ujerumani.
Wanaowania tuzo ya kocha bora kwa wanaume ni Luis Enrique García, wa Barcelona, Pep Guardiola wa Bayern Munich na Jorge Sampaoli kocha wa timu ya taifa ya Chile.
Wanaowania tuzo ya kocha bora kwa wanawake ni Jill Ellis kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Mark Sampson kocha wa timu Uingereza na Norio Sasaki anayeifunza timu ya Japan.
Tuzo ya bao bora la mwaka maarufu kama Puskas inawaniwa na Alessandro Florenzi wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya As Roma, Wendell Lira Mbrazil anayechezea klabu ya Vila Nova na nyota wa Barcelona Lionel Messi
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo