Waziri mkuu wa zamani Ufaransa ajitosa kuwania urais 2027
4 Septemba 2024Matangazo
Bado Rais Emmanuel Macron anahangaika kutafuta waziri mkuu mpya tangu aliposhindwa kukiimarisha chama chake kupitia uchaguzi wa bunge uliofanyika mwezi Julai.
Kushindwa kwa chama chake kumesababisha mkwamo wa kisiasa huku muungano wa mrengo wa kushoto ukihodhi idadi kubwa ya viti katika bunge ambalo halina mshindi wa moja kwa moja.
Soma pia:Macron aongeza juhudi za kuvunja mkwamo wa kisiasa
Wakati mazungumzo ya kuumaliza mkwamo wa kisiasa yakiendelea waziri mkuu wa zamani Eduardo Phillipe amethibitisha atagombea urais kurithi nafasi ya Macron, ambaye hawezi kugombea tena mwaka 2027 muhula wake wa pili utakapofikia mwisho.